| |

By Webmaster 1 Replies
|
MTUMIE KADO UPATE USINGIZI. On 2009-11-11 21:06:28 Kufuatia kucheza vibaya kwa magolikipa wanaoteuliwa na mwalimu Marcio Maximo kwenye kikosi cha timu ya taifa huku wapenzi wengi wa mpira nchini wakiendelea kumlilia Juma Kaseja sakata la golikipa anayetakiwa kusimama kwenye milingoti mitatu ya timu ya taifa linaendelea kuwa zogo kila kukicha Maximo anaonekana kuziba masikio na hataki kuyamaliza na Kaseja ili kumrejesha golikipa huyu kipenzi cha watanzania Stars lakini webmaster wa mtibwasugar.com analo wazo kwa maximo.... MTUMIE KADO UPATE USINGIZI.
webmaster anaamini kuwa endapo Maximo atamtumia Shaabani Kado, basi bila shaka atapata usingizi toka kwa wanaompinga kwani uwezo wa Kado kwa sasa ni wa kiwango cha juu na hauna tofauti na kaseja. Kado anaaminika kuwa ndiye golikipa bora kabisa nchini kwa sasa, mshindi huyu wa tuzo la golikipa bora mwaka jana ambaye ameingongoza Mtibwa Sugar kushika nafasi ya pili kwenye ligi kuu huku ikitwaa kombe la Tusker na Ngao ya Hisani ana kila sifa na Maximo hana budi kumtumia kama golikipa wake namba moja kwa sasa
changia mawazo yako hapa
|
|
|