Taifa Stars uso kwa uso na mbweha wa Jangwa leo
Posted on Sat 12th June 2010 12. 23PM by Webmaster
|
| Stars Mazoezini |
Taifa Stars uso kwa uso na mbweha wa Jangwa leo
Na Florian Kaijage
Algiers Algeria
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Ijumaa usiku inashuka dimbani kwenye uwanja wa wa Tshaker katika kitongoji cha Blida jijini hapa kukabiliana na wenyeji wao ‘Mbweha wa Jangwa’ Algeria katika mchezo wa kwanza wa kundi ‘D’ Kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 2012 zitakazofanyika Gabon na Equatorial Guinea. Mchezo utaanza saa nne kamili za hapa sawa na saa 6 za Afrika Mashariki.
Taifa Stars chini ya mkufunzi wake Ja n Poulsen kutoka Denmark iliwasili hapa Algiers Jumatano mchana na Alhamis usiku kikosi hicho kwanza ambayo Poulse amesema yamekwenda vizuri kama alivyopanga na kwamba yanatia matumaini.
Poulsen, ambaye anajivunia rekodi ya kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 1992 akiwa kocha msaidizi wa Denmark atakuwa akikiongoza kikosi cha Taifa Stars katika mchezo wa pili na wa kwanza wa kimashindano tangu aanze kufanya kazi hiyo Agosti mosi na kasha kupata sare ya 1-1 dhidi ya Kenya katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki Agosti 11 mwka huu jijini Dar es Salaam.
Shinikizo kubwa litakuwa kwa Algeria, wao ni wenyeji wa mchezo huu, wanao wachezaji wakubwa ambao wanacheza katika klabu za ligi maarufu duniani zikiwemo Ujerumani, Ufaransa, England, Italia na nyingiezo na pia wanapewa nafasi kubwa kuliko sisi ambao wengi wa ntuoa ni wanyonge tu’ alisema kocha huyo ambaye aliiwezesha Jordan kufuzu kwa fainali za dunia FIFA za umri chuni ya miaka 20 huko Canada mwak 2007.
Akaongeza ‘wachezaji wangu wanaonekana wana ari kubwa, wan hamu ya kufanya vizuri wanajituma a iwapo tulivyofanya mazoezini tutafanya hivyo katika mchezo sina shaka tutapata matokeo ya kurejea nayo nyumbani’.
‘Hata hivyo lazima tufanye kazi ya kwelikweli, ni muhimu kila moja atekeleze majukumu yake uwanjani kwani tutalazimika kukimbia sana kumili uwezo a shinikizo za wapinzani a muhimu zaidi lazima tulinde sote lango letu tunapopoteza mpira na kushambulia kwa kasi tuanapokuwa na mpira, tukitekeleza haya tutakuwa katika hali nzuri kimchezo’ alisisitiza Poulsen.
Kuhusu kujiamini kwa wachzeji wake, Poulsen anasema hanatatizo na hilo na kwamba anaamini hali nzuri ya kisaiklojia na kutokuwa na woga kumetokana a Taifa Stars kupata fursa nzuri ya kucheza na wachezaji wa timu bora duniani kama vile Brazil, Ivory Coast na Cameroon.
Amesema anafahamu Algeria wanao wqachezaji maarufu kama vile Karim Matmour anayekipiga katika klabu ya Brossia Monchegladbach ya Ujerumani lakini akasema Matmour jina kubwa si kama la Ricardo Kaka wa Brazil au Didier Drogba wa Ivory Coast ambaye tayari wachezajiw Taifa Stars wamewakabili vilivyo.
Amesifu mchango wa wachezaji wa wanaokipiga nje ya Tanzania kuwa ni muhimu kwa timu kwani ya kuwa na kujitambua pia wamekwishapita katika mazigira mengi ikiwemo mifumo tofauti ya kiuchezaji a hivyo kuwafanya wawe katika haki nzuri zaidi kiushindani. Wachezaji wa Stars wanaocheza nje ni pamoja na Nizar Khlafan wa klabu ya Vancouver Whitecaps ya Canada, Henry Joseph wa Kongsvnger IL ya Norway, Idrisa Rajabu wa Sofapaka ya Kenya na Danny Mrwanda wa DT Long An ya Vietnam.
Mchezo huu utachezeshwa na waamuzi kutoka Togo amabpo mwamuzi wa kati ni Djaoupe Kokou atakayesaidiwa na Djoukere Biagui na Ayena Mathias na mwamuzi wa akiba ni Bougounou Fabrice.
Kwa mujibu wa mazoezi ya Jumatano kikozi cha kwanza kinaweza kuwa hivi:
Shaaban Hassan ‘Kado’ Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika, Agrey Morris, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Henry Joseph, Mrisho Ngasa, Abdi Kassim, Danny Mrwanda, Nizar Khalfan na Idrissa Rajabu.
Kikosi cha Algeria
Kikosi cha Algeria ambao ni mabingwa wa Afrika wa mwaka 1990, kinaolewana kocha mzawa Rabah Saadane ambaye amekuwa akiteuliwa na,kuondolewa mara kadhaa kwenye timu hiyo tangu alipoteuliwa kwa ,mara kwanza kuwa kocha msaidizi mwka 1982.
Kocha huyo ambaye amekuwa akikinoa kikosi hicho kwa miaka 8 sasa anawategemea zaidi wachezaji wake wanaokipiga Ulaya.
Hao ni pamoja na Majid Bougherra wa Rangers ya Scotland, Nadir Belhaji wa Al Saad ya Sudia Arabia, Rafik Halliche ambaye amehamia Fulham ya England akitokea Benfica ya Ureno, Rafik Djebbour wa EAK Athens ya Ugiriki, Hassan Yebda wa Benfica na Ryad Bouadebouz wa Sochaux ya Ufaransa.
Wengine ni Habib Bellaid wa Entracht Frankfurt ya Ujerumani, Abdelkader Gezzal wa Bari ya Italia Djamal Abdouni wa Nantes ya Ufaransa, Andlane Guedoura wa Wolves ya England na Karim Ziani wa Wolsburg ya Ujerumani.
Wchezaji muhimu watakaokoseka ni pamoja na mlinda lango namba moja Rais Mbholi Slavia Sofia ya Bugaria na mlinzi Anther Yahia wa Bochum ya Ujerumani.
Vyombo vya habari vya Algeria
Vyombo vya habari vya hapa vimekuwa vikichapisha habari nyingi zikitahadhalisha timu yao kuwa wasifaya kosa la kuidharau Tanzania japo wanaonekana kukosa habari nyingi juu ya Taifa Stars.
Baada ya timu kuwasili waandishiow a habari wa Televisheni ya Taifa ya Algeria walionekana kuwafuatilia zaidi wachezaji wanaocheza nje ya Tanzania huku wakitaka kuwapiga picha Nizar Khalfan na Henry Joseph.
Wachezaji wengine ambao waandishi hao walitaka kufahamu habari zao a kuwahoji I pamoja na Mrisho Ngasa ambaye ndiye mshambulaaji anayeongoza kwa kupachika mabao pamoja na mlizi Nadir Haroub “Cannavaro’. Hata hivo jitihada hizo za kuwahoji wachezaji hao zilizimwa na viongozi wa timu kwani zilionekana zaidi kutaka kuwavuruga wachezaji kisaiklojia.
Gazeti la kila siku lichapishwalo kwa lugha ya Kifaransa liitwalo La Tribune limechapisha kikosi kizima cha Stars kilichopo hapa bila kuwa na dondoo kitapangwa vipi.
Vilevile waandishi na wapiga picha wa Televisheni ya Taifa ya Algeria walifika kinyemera katika mazoezi ya Stars Jumatano usiku huku wakitaka kurekodi mazoezi hayo, mpango ambao hata hivyo ulishtukiwa na kuzuiwa.
Ilibidi mpiga picha ambaye jina lake halikupatikana mara moja anyang’anywe DVD aliyokuwa ndani ya Camera kwani viongozi wa timu walikuwa na wasiwasi kuwa alikuwa amerekodi sehemu ya mazoezi ya Stars.
Rekodi ya kimashindano kati ya Ageria na Tanzania
Algeria na Tanzania zimewahi kucheza michezo miwili tu ya kimashidano hiyo ilikuwa mwaka 1995 wakati nchi hizo zilpokuwa kundi moja katika kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za Afrika za mwaka 1996 zilizofanyika Afrika Kusini.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Januari jijini Dar es Salaam Taifa Stars chini ya ukufunzi wa Sunday Kayuni iliibwaga Algeria 2-1 moja ya magoli ya Stars likifungwa na Juma Bakari Kidishi.
Hata hivyo katika mchezo wa marudiano uliofanyika Julai 1995 Algeria walishinda 2-1 katika mchezo ulichezwa kwenye uwanja wa Julai 5 jijini Algiers.
Timu hizo ziliwahi pia kukutana katika michezo miwili ya kirafiki mwaka 1997 wakati Algeria ilipoalikwa kushiriki sherehe za ufunguzi wa uwanja wa Taifa (Sasa uwanja wa Uhuru) uliokuwa umekarabatiwa. Mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya 1-1 na katika mchezo wa pili Algeria walishinda 1-0.